.

.

.

.

Thursday, February 19, 2009

MAUAJI YA KIKATILI YA ALBINO SENGEREMA !!!


SAMAHANI KWA PICHA HII YA KUSIKITISHA

SAKATA la mauaji ya kinyama dhidi ya msichana mwenye ulemavu wa ngozi (Albino)wilayani Sengerema mkoani mwanza limeingia katika sura mpya,baada ya mdogo wa marehemu kudai kuwa baba yake mzazi alikuja na watuhumiwa kutoka kwenye kilabu cha pombe na wanaodaiwa kumuua na kasha kumnyofoa miguu yote miwili Dada yake.

Akizungumza na Mwandishi wa habari hii katika eneo la tukio Mtoto huyo Leticia Bahati(8)ambaye ni mwanafunzi wa darasa la kwanza katika shule ya msingi ya Kashindaga,alisema kuwa siku ya tukio majira ya usiku ambayo hakuweza kujua ilikuwa ni saa ngapi,baba yake mzazi alikuja na kuwaamsha ili wamfungulie mlango.Alisema kwa kuwa yeye na Dada yake ambaye sasa ni marehemu walikuwa wamelala sebuleni tena mlangoni walikuwa wa kwanza kuamka na kumfungulia mlango Baba yao,ambapo kabla ya kuingia ndani ya nyumba alisikia baba yake akizungumza na watu nje ya nyumba ingawa hakuweza kujua ni watu w aina gani.
‘Aligonga mlango na dada akamfungulia kwa sababu sisi tulikuwa tumelala sebuleni karibu kabisa na mlango,lakini kabla ya baba kuingia ndani mimi na dada tulisikia baba akizungumza na watu nje ya nyumba hatukufuatilia kwa sababu tulijua labda ni marafiki zake kwa sababu mara nyingi huwa anakuja usiku lakini siku hiyo alikuwa amechelewa sana………’’ alisema mtoto huyo.

Huku akizungumza kwa lugha ya kisukuma mtoto huyo alisisitiza kuwa……….Akiza bababotiku….ogonga nyango,tomwigolela aho atale kwengela twigwa aleyomba na banho hanze aleyo tolabhatebhile………’’(alikuja baba usiku akagonga mlango tukamfungulia lakini kabla hajaingia ndani ya nyumba tukamsikia akizungumza na watu nje ambao hata hivyo hatukuwajua)….’.
Alibainisha kuwa baada ya baba yake kuingia ndani ya nyumba Dada yake ambaye ni marehemu alimtengea chakula chumbani alipokuwa amelala mama yake,na kisha wao kurejea kulala ambapo baada ya muda mfupi ndipo walipovamiwa na dada yake kuuawa kabla ya kunyofolewa miguu yote miwili na watu ambao hakufanikiwa kuwaona kutokana na kulazimishwa kulala kifudifudi.

Mtoto huyo ambaye alikatwa sehemu ya kidole gumba chake cha mguu wa kulia na panga wakati marehemu dada yake akinyofolewa miguu kutokana kulala karibu naye,alisema watu hao walikuwa wamejifunga vitambaa vyeusi usoni kwa ajili ya kuficha nyuso zao na kwamba kabla ya kumlaza kifudifudi walimpiga na ubapa wa panga mgongoni.
Alisema siku hiyo dada yake aliamua kulala sebule na kukataa kulala chumbani pamoja na wenzake kutokana na wadudu aina ya kunguni ambao walikuwa wakiwauma sana,ambapo naye aliamua kwenda kulala na dada yake sebuleni kabla ya kukumbwa na mkasa huo usiku.

Hata hivyo akizungumza na muda mfupi kabla ya kutiwa mbaroni Baba Mzazi wa Mtoto huyo Bahati Lugwisha (53)alikiri kurudi usiku siku hiyo tofauti na siku zingine,kwa maelezo kuwa alikuwa akinywa pombe katika kilabu cha mtu mmoja wa kijijini hapo aliyemtaja kwa jina moja na Simon pamoja na rafiki zake.
Tayari jeshi la polisi linawashikilia watu wanane akiwemo Baba mzazi wa mtoto huyo kwa tuhuma za kuhusika katika mauaji ya kinyama dhidi ya msichana huyo,ambapo habari kutoka ndani ya jeshi la polisi wilayani Sengerema zinaeleza kuwa bado polisi inaendelea na msako dhidi ya watuhumiwa wengine wanaodaiwa kutoroka kutoka kijijini hapo mara baada ya kutokea kwa tukio hilo.

JE ? WAZIRI MKUU ALIPOLIA BUNGENI KWA AJILI YA VIUMBE HAWA KWA NINI HAIKUELEWEKA KWA VIONGOZI WENGINE ???

No comments:

Post a Comment